November 22, 2015


Chama cha mapinduzi CCM kimesema ndoto za mchana Maalim Seif kuapishwa kuwa Rais wa Zanzibar kwani Tume ya Uchaguzi Zanzibar tayari imeshatangaza kufutwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika novemba 25 mwaka huu 2015.
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, CCM Zanzibar Waride Bakari Jabu amesema mawazo hayo ya wana CUF ni kuwadanganya wananchi wakati wanafahamu hali halisi ilivyo.
CCM pia imelaani kitendo cha wabunge wa kambi ya upinzani wanaounda ukawa kuwazomea viongozi wakuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wakiingia katika ukumbi wa Bunge Dodoma.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa afisi kuu ya CCM Kiswandui Waride amesema kitendo hicho ni ukosefu wa nidhamu.
Kwa kweli tabia ile si taba ya kiungwana lakini pia walikusudia kuwavunjia heshima viongozi wakuu wa SMZ pamoja na kuwasumbua wananchi kusikiliza hotuba ya rais wa jamburi ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli alipolizindua bunge la 11” amesema Waride.
ameahamisha kuwa hayo sio matarajio ya chama cha mapinduzi kilichoridhia mfumo wa vyama vingi vya siasa pamoja na kuundwa kwa serikali ya Zanzibar yenye mfumo wa umoja wa kitaifa.



0 comments:

Post a Comment