November 21, 2015

Tume ya kurekebisha sheria Zanzibar imesema imeshaandaa mkakati wa kuzifanyia marekebisho sheria mbali mbali zenye mapungufu ili ziendane na mazingira ya sasa.
Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mshibe Ali Bakari
amesema mabadiliko katika sekta ya sheria yanalenga kuleta  ufanisi na kutoa usimamizi bora.
Amesema hatua hiyo itafanikisha jamii kuwa  na uelewa na utii  wa sheria huku ikirahisisha usimamizi wake.
Akifungua mafunzo ya kupitia mkakati huo  mjini Zanzibar amesema lengo ni kuweka maadili kwa watendaji wakuu wa taasisi  pamoja na  kuwawezesha kusimamia mabadiliko hayo.
Akitoa mada katika mafunzo hayo Mhadhiri wa chuo Kikuu cha Mzumbe Dkt  Julius Cosmas  amesema mfumo mbaya wa sheria na vitendo vya rushwa Zanzibar umechangia kukwama kwa maendeleo katika sekta zote.

0 comments:

Post a Comment