November 30, 2015


Chama cha mapinduzi CCM Zanzibar kimekanusha taarifa zilisambazwa katika mitandao ya kijamii zinazohusiana kuwa chama hicho kimeridhia kuapishwa kwa maalim Seif kuwa rais wa Zanzibar.
Naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai amesema kauli hizo hazina ukweli na ni  mpango maalum wenye nia ya kuvuruga amani ya nchi .
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu ya CCM  Kisiwandui mijini Zanzibar amesema lengo la taarifa hizo ni wanaccm na wapenda amani wasiweze kuendelea na shughuli zao za kujiletea maendeleo.
 Amefahamisha kuwa kwa sasa mazungumzo yanaendelea ya kutafuta suluhu ya mkwamo wa kisiasa Zanzibar kati ya Dk Shein na Maalim Seif na Marais wastaafu wa Zanzibar hivyo  amewataka  wanaccm kuwa wastahamilivu.

0 comments:

Post a Comment