November 30, 2015


Mahakama ya rufaa ya Tanzania imeanza kazi ya kusikiliza mashauri 21 ya kesi za rufaa upande wa Zanzibar na kutolewa  uamuzi.
Mashauri hayo yatasikilizwa katika mahakama kuu ya Zanzibar ni pamoja na kesi za madai na jinai.
Akitoa ufanunuzi  jaji  Mkuu wa Tanzania  jaji Mohammed  Chande Othaman  juu ya  mashauri amesema watasikiliza kesi hizo kuanzia sasa hadi Disemba 14.
amesema kati ya mashauri hayo yatakayosikilizwa  mengi  ni ya madai  na matatu yatakuwa  ya kesi za jinai.
Jaji Chande amefahamisha kuwa  mashauri hayo  ni wadai na wadaiwa  na wamekuwa na mawakili wa kuwakilisha katika kesi  ikiwa  ni utaratibu  uliyowekwa  katika mahakama ya rufaa.
Ameeleza kuwa mahakama ya rufaa itahakikisha  kila mmoja  anapata fursa ya kutumia haki yake kwa mujibu wa sheria.   
Kikao hicho cha kwanza cha mahakama ya rufaa kilitanguliwa na ufunguzi wa gwaride  kuashiria kuanza kwa vikao. 

0 comments:

Post a Comment