Mahakama ya hakimu mkazi Morogoro imemuachia huru Katibu wa
Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa
akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya upande wa mashtaka wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka
yaliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi yake.
Sheikh ponda alikuwa anakabiliwa na makosa mawili ikiwemo kushawishi
watu kutenda kosa, pamoja na kutoa matamshi yanayoumiza imani ya dini nyingine amekaa rumandae kwa zaidi ya miaka miwili kutokana
na kuzuiliwa dhamana yake kwa maslahi ya taifa.
Hakimu wa kesi hiyo Mary Moyo amesema ushahidi uliotolewa na
upande wa mashitaka haukujitosheleza hivyo mahakama hiyo imemwachia huru na
rufaa iko wazi endapo upande wa mashitaka hautaridhika.
Akizungumza
baada ya kuachiliwa huru sheikh ponda ameishukuru mahakama kwa kutenda hakijapo
kuwa imechelewa kutoa hukumu.
0 comments:
Post a Comment