Meli mpya ya Serikali ya Zanzibar Mv Mapinduzi II inatarajiwa kufika Zanzibar Disemba 2 mwaka huu baada ya kumalizika kwa matengenezo yake.
Meli hiyo imetengenezwa Korea ya kusini kwa gharama ya dola za Kimarekeni milioni 30.6 ilitarajiwa kuwasili Zanzibar mwezi Julai 2015 lakini imechelewa baada ya kuwekewa kuzuizi na kampuni moja ya Leomthong ya Thailand.
Kampuni hiyo ilikuwa inaidai Shirika la Biashara za Nje Zanzibar BIZANJE lililokuwa likiingiza vyakula na bidhaa mbalimbali katika miaka ya 80.
Katibu Mkuu wizara ya Fedha Khamis Omar amesema kufuaitia zuia hilo walifungua kesi mahakani kwa kuwa madai hayo hayakuwa na sasa meli ya MV Mapinduzi II ipo njia baada ya kuanza safari ya kuja Zanzibar kutoka Mauritius tangu Novemba 26.
Meli hiyo inachukuwa nafasi ya meli ya mwanzo MV Mapinduzi iliyotengenezwa chini ya utawala wa Rais Aboud Jumbe Mwinyi iliyouzwa mwaka 2011 na ilizama katika bahari ya visiwa vya Sychelles ikiwa ikielekea nchini Yemen kwa ajili ya matengenezo mara baada ya kuuzwa.
0 comments:
Post a Comment