Mapungufu ya kisheria ni miongoni mwa vikwazo
vinavyosababisha kuwepo na ugumu wa watuhumiwa wa kesi za udhalilishaji kutiwa
hatiani zanzibar.
Sheria hizo pamoja na ya ushahidi
ya mwaka 1917 sheria mwenendo wa makosa ya jinai no 6 ya mwaka 2006
na kukosekana sheria ya kuzuia udhalilishaji kwa njia ya elektroniki.
Mkurugenzi Idara ya Mashtaka Zanzibar
Ibrahim Mzee Ibrahim amesema mapungufu hayo wakati mwengine hutumika kumaliza kesi
nyingi bila ya kutoa haki.
“ Kwa mfano sheria ya ushahidi ya
mwaka 1917 ni ya zamani sana inahitaji marekebisho makubwa ili kwenda na wakati”
amewaambia waandishi wa habari waliofika ofisini kwake .
Hata hivyo amesema wameshapendekeza Tume ya
marekebisho ya sheria mapungufu hayo ili
kufanyiwa kazi kwa mujibu wa wakati.
Mkurugenzi Ibarahim ameiomba
jamii kutoyafumbia macho makosa ya udhalilishaji na kuwa tayari kutoa ushahidi
pale unapohitajika.
“Mtu yoyote atakaeona kesi yake
inakwenda vibaya iwe polisi au mahakamani ni vizuri kufika hapa (afisi ya
mkurugenzi wa mashtaka) na tutamsaidia kwa mujibu wa sheria bila ya vikwazo.
0 comments:
Post a Comment