April 30, 2014


Taasisi zinazosimamia uharibifu wa mazingira Zanzibar zimetakiwa kushirikiana na kufanya kazi kitaamu katika kukabiliana na  athari za kimazingira.

Mwenyekiti wa kamati ya inayosimamia viongozi wakuu wa kitaifa Hamza Hassan Juma amesema ufanyakazi kwa mazoea umepitwa mazingra na kinachohitajika zaidi ni utendaji wa kitaalamu katika  harakati za kusimamia mazingira ya nchi.

Alikuwa akizungumza katika zaira maalum ya kuangalia baadhi ya maeneo yaliyoathirika na mvua za  masika zilizonyesha hivi karibuni ikiwemo Mwanakwerekwe, Daraja bovu, Chumbuni na Kiazini mjini Unguja.

Mkurugenzi wa Idara ya mazingira Sheha Majaja amesema ujenzi unaoendelea katika eneo  linalojaa maji la Chumbuni kwa Mzushi linahitaji uangalifu kwani unaathari kubwa kwa wananchi wanaoishi eneo hilo hasa wakati wa mvua kubwa.

Wakati huo huo kamati ya kudumu ya mawasiliano na ujenzi ya baraza la wawakilishi imeiomba mamlaka ya maji Zanzibar ZAWA  kuweka mikakati itayosaidia kuongeza  kiwango cha upatikanaji maji safi kwa wananchi.

Kamati hiyo imaishauri zawa kuendelea kutoa taaluma uhifadhi wa mazingira kwa wananchi wanaoishi karaibu na vianzio vya maji.

Kamati hiyo ilitembelea vianzio vya maji vya Mwanakwerekwe, Tunguu, Machui, Chumbuni na Mwanyanya  vinavyoimarishwa kwa ufadhili wa  serikalii ya Ras-el-Khaimah pamoja na Benki ya maendeleo ya Afrika.

0 comments:

Post a Comment