Benki ya watu wa
Zanzibar PBZ imepata faida ya shilingi bilioni 7 ikiwa ni mara tatu zaidi ya faida
ya makusanyo yake .
Mkurugenzi
mtendaji wa PBZ Juma Amour amesema makusanyo hayo ni ya jumla bila ya kodi Na mi
hatua muhimu kwa maendeleo ya banki hiyo yanayoimarika kila siku.
Akizungumza
katika hafla ya kumuaga msaidizi wa Mkurugenzi Ame Haji Makame anaemaliza muda
wake wa utumishi wa umma iliyowashirikisha wajumbe wa bodi na maafisa wa benki
hiyo amesema mafaniko hayo yamechangiwa na utoaji huduma bora kwa wananchi.
Nae Mwenyekiti
wa bodi ya PBZ amefahamisha kuwa benki
hiyo inathamini mchango wa mstaafu huyo alietumika taasisi hiyo kwa kipindi cha
miaka 40 na aliesaidia kufikia mafaniko hayo.
Kwa upande wake Ame
Haji Makame ameushukuru uogozi na wafanyakazi hao kwa ushirikiano wao na
kuwataka wafanyakazi kukinai na maslahi wanayoyapata katika utendaji wa kazi
zao.
eMwenyekiti wa bodi ya PBZ Mwinyi Mbegu |
Mzee Ame Haji Makame akitoa shukurani kwa wafanyakazi wenzake wa PBZ
|
0 comments:
Post a Comment