Serikali imetakiwa kutenga bajeti maalum kwa Kamisheni ya utalii Zanzibar ili kuweza kushughulikia nyumba za kulaza wageni zilizokuwa hazijasajiliwa (gesti bubu) zinazoendelea kuongezeka katika maeneo mbali mbali ya kiutalii Mjini na Vijijini.
Mwenyekiti wa kamisheni hiyo Dr Ahmada Hamadi Khatib amesema Zanzibar inakusanya zaidi ya Shilingi Bilioni 2 kupitia leseni za kuendesha shughuli za utalii hivyo kuendelea kwa biashara ya magesti bubu kunahatarisha kupungua mapato ya Serikali.
Ameyataja maeneo yaliyoongezeka nyumba hizo ni mji Mkongwe, Nungwi, Kizimkazi na maeneo ya Paje na Jambiani mkoa wa kusini unguja.
Dr. Khatib ameongeza pia nyumba hizo pia zinachangia kuipotezea sifa ya Zanzibar kiutalii kutokana kukosa viwango bora vya utoaji huduma ikiwemo kuhatarisha usalama na afya za wageni za wageni.
Ameelezea muhimu wa serikali kuweka kipaumbela cha upatikanaji wa fedha hizo ili kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kubaini wanaoendelea kufanya biashara ya kulaza wageni kinyume cha sheria .
0 comments:
Post a Comment