Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) inatarajia kujenga Bara bara Nne zenye urefu wa
Kilomita 51.78 katika azma yake ya kuimarisha sekta ya mawasiliano ya usafiri
wa ardhini hapa Nchini.
Ujenzi wa
Bara bara hizo Nne za Zanzibar unajumuisha sambamba na zile za
Tanzania Bara zitakazopata msukumo wa ufadhili kupitia Mfuko huo wa Benki
hiyo ya Maendeleo ya Afrika zote zikiwa na urefu wa Kilomita Mia 462.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo kwenye Warsha
ya uzinduzi wa Mradi wa Mpango wa uimarishaji wa
Sekta ya Usafiri (TSSP)
iliyofanyika Zanzibar Beach Resort
Mazizini nje kidogo ya Mji wa Zanzibar na kushirikisha wataalamu wa sekta ya
usafiri, watendaji wa Serikali pamoja na wawakilishi wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika.
Balozi
Seif alisema mradi wa Bara hizo ni pamoja na zile za Bububu – Mahonda – hadi
Mkokotoni wenye wenye urefu wa Kilomita 31, Pale – Kiongele Kilomita 4.6,
Fuoni – Kombeni Kilomita 8.6 na Matemwe – Muyuni Kilomita 7.6.
Alisema
ushirikiano wa karibu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na washirika
wa maendeleo umeiwezesha miundombinu ya bara bara zenye urefu wa Kilomita
90 kuimarika ndani ya kipindi cha miaka Mitano iliyopita zikiwa katika
kiwango kinachokubalika Kimataifa .
Alifahamisha
kwamba Serikali kupitia mfuko wa Bara bara Zanzibar (ZRF) iliongeza bajeti
yake kwa ajili ya matengenezo ya Bara bara kutoka shilingi Bilioni 5
mwaka 2011 hadi shilingi Bilioni 7.3 mwaka uliopita wa 2015.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba kuanza kwa miradi hiyo ya ujenzi wa
Bara bara za Zanzibar kwa upande mwengine kutatoa fursa za ajira 1,500
kwa baadhi ya wananchi hasa Vijana.
Alisema
fursa hizo pia zitaibua ajira za muda zipatazo 3,000 katika kazi za
matengenezo ya bara bara zinazoharibika kutokana na matumizi mbali mbali
ikiwemo kuharibika kwa mvua.
Balozi
Seif aliupongeza Uongozi na Watendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika chini ya
usimamizi wa Mwakilishi wake hapa Nchini Dr. Tonia Kandiero kwa juhudi
wanazochukuwa katika kusaidia Maendeleo ya Nchi changa hasa zile zilizomo
katika ukanda wa jangwa la sahara.
Alisema
mbali ya kuunga mkono nguvu za uimarishaji wa sekta ya Bara bara lakini pia
Benki hiyo imeonyesha nia yake thabiti ya kusaidia uendelezaji wa miradi mbali
mbali ya maendeleo na ustawi wa jamii nchini.
Balozi
Seif alisema ipo miradi ya Afya, Elimu, Kilimo, Huduma za Maji safi na salama
pamoja na mafunzo ya kuijengea Jamii namna ya kuishi katika misingi ya utawala
Bora ambayo imepata msukumo wa Benki hiyo kupitia Mpango wa kuunga mkono
Sekta ya Usafiri (TSSP).
“ Benki ya
Maendeleo ya Afrika imeanza kutoa huduma zake Zanzibar tokea mwaka 1998
kwa kusaidia ujenzi wa Bara bara Tano zenye urefu wa Kilomita 88.3 ambazo
ni Kinyasini – tunguu, Paje – Makunduchi, Mazizini – Fumba na Amani – Dunga ”.
Alifafanua Balozi Seif.
Mapema
kaimu mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bibi Merry Helen Minja alisema
Taasisi hiyo ya kifedha kwa maendeleo ya Mataifa ya Bara la Afrika imejikita
zaidi katika kuona mipango ya Mataifa hayo kama ile ya kupunguza Umaskini (MKUZA na MKUKUTA) inafanikiwa vyema.
Bibi Minja
alisema Mradi wa Mpango wa uimarishaji wa Sekta ya
Usafiri (TSSP)
umeanza kubuniwa rasmi Tarehe 26 Novemba mwaka 2015 na kufikia hatua ya kuwekwa
saini mkataba wake mnamo tarehe 4 Disemba mwaka 2015.
Kaimu
Mwakilishi huyo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bibi Merry Helen Minja
alifahamisha kwamba mradi mzima wa ujenzi wa bara hizo unatarajiwa kugharimu
jumla ya Dola za Kimarekani Milioni 270.95 sawa na shilingi Trilioni 1.3za
Kitanzania.
Akimkaribisha
mgeni rasmi kuzindua Mradi huo wa Mpango wa uimarishaji wa
Sekta ya Usafiri (TSSP)
Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano
Zanzibar Dr. Juma Malik Akio alisema kwamba maendeleo ya Taifa lolote duniani
hutegemea kuimarika kwa Sekta ya mawasiliano ya usafiri.
Dr. Malik
alisema Wizara anayoisimamia imepewa jukumu la kusimamia jukumu hilo kazi
ambayo imekuwa ikipata mafanikio kutokana na nguvu ya pamoja kati ya
Serikali na washirika wa maendeleo ndani na nje ya Nchi.
Warsha
hiyo ya siku moja ya uzinduzi wa Mradi wa Mpango wa
uimarishaji wa Sekta ya Usafiri imejadili mada Nne muhimu miongoni
mwake ni pamoja na sheria na taratibu za manunuzi, ujenzi wa bara bara zilizomo
ndani ya mradi huo pamoja na ripoti ya fedha na ukaguzi wake.
Kaimu Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Bibi Merry
Helen Minja
akifafanua hatua zitakazochukuliwa katika hatua za
utekelezaji wa Mradi
wa mpango wa uimarishaji wa sekta ya usafiri
. |
Balozi Seif aliyepo kati kati ya waliokaa vitini akiwa
katika picha ya
pamoja washiriki wa warsha
ya uzinduzi wa Mradi wa Mpango wa
uimarishaji wa Sekta ya Usafiri.
|
0 comments:
Post a Comment