Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, imetiliana saini na Serikali ya Sweden makubaliano
ya kuimarisha huduma za nishati ya umeme hapa nchini.
Katika
hafla ya utiaji saini wa mradi huo, Zanzibar iliwakikishwa na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na Makaazi Ali Khalil Mirza, wakati
Makamu wa Rais Mtendaji wa Kampuni ya Multi Consult kutoka Norway Oyvind
Holtedahl, alisaini kwa niaba ya Serikali ya Sweden.
Katika
hafla hiyo iliyofanyika Makao makuu ya Wizara ya Maji, Ardhi, Nishati na
Makaazi Katibu Mkuu Mirza, alisema kampuni ya Multi Cionsult ilishinda
zabuni hiyo kati ya kampuni 12 zilizoomba kutekeleza mradi huo.
Alieleza
kuwa mradi huo utakaochukua miaka mitatu na nusu hadi kukamilika kwake,
utagharimu shilingi bilioni 12.7 za Kitanzania.
Amefahamisha
kuwa, miongoni mwa matumizi ya fedha hizo, ni kuwapatia mafunzo wafanyakazi wa
wizara hiyo ili kuwajengea uwezo wa kufanya tafiti ili wafanye kazi zao kwa
ufanisi.
Mirza
alieleza kuwa, lengo la Kampuni hiyo ni kusaidia katika kulijengea uwezo
Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) pamoja na Idara zake kuhusu sera ya nishati
ambayo ni muhimu kwa maenedeleo ya taifa.
Naye
Mshauri Mwandamizi wa Kampuni ya Multi Consult ameishukuru Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwaamini kufanya kazi hiyo na ameahidi kuwa wataitekeleza
kwa ufanisi mkubwa.
:Melezo Zanzibar
0 comments:
Post a Comment