March 06, 2016

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameongoza mamia ya wananchi  na viongozi katika maziko ya marehemu Mzee Hamid Ameir muasisi wa mapinduzi.
Marehemu Mzee Ameir aliekuwa pia Mwenyekiti wa baraza la wazee wa CCM ameezikwa leo kijijini kwao Donge wilaya ya kaskazini B.Unguja.
Alifariki jana katika hospitali ya Mnazi mmoja alipokuwa amelazwa kwa matibabu.

Mungu amlaze mahala pema peponi AAMIN.


Waziri wa nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohammed Aboud Mohammed
 akisoma risala ya na wasifu wa Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa 
Mapinduzi, pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM  baada ya kuzikwa
 leo  Kijijini kwao Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.  
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
 (katikati) pamoja na Viongozi wengine na wananchi wakiitikia dua iliyoombwa
 baada ya kuzikwa Marehemu Mzee Hamid Ameir Muasisi wa Mapinduzi,
pia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa CCM leo Kijijini kwao 
Donge wilaya ya Kaskazini B.Unguja.



0 comments:

Post a Comment