Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo jioni (Ijumaa, Februari 19,
2016) amekagua bandari ya Tanga na kumtaka Mkuu wa Bandari ya Tanga (Port
Master), Bw. Henry Arika amletee maelezo juu ya ukiukwaji wa manunuzi ya
tishari ifikapo kesho (Jumamosi) saa 6 mchana.
Waziri Mkuu ambaye aliwasili Tanga kushiriki
mazishi ya baba mzazi wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Bi. Ummy Mwalimu yaliyofanyika kwenye makaburi ya Mchukuuni, Tanga,
aliamua kuzuru bandari hiyo kabla ya kuelekea uwanja wa ndege akiwa njia njiani
kurejea Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo fupi, Waziri Mkuu alikataa kuingia ofisini (bandarini) na akataka apelekwe mahali tishali tatu za bandari hiyo zilipo. Katika maswali aliyoulizwa na Waziri Mkuu, Bw. Arika alikiri kuwa matishari hayo hayafanyi kazi kama inavyotakiwa kwa sababu yanasubiri kusukumwa na tugboat (meli ndogo).

"Nataka kesho saa 6 mchana uniletee barua yenye maelezo
ni kwa nini mlinunua tishali tatu ndogo badala ya mbiili kubwa wakati mnajua
Serikali ilitenga Dola za Marekani milioni 10.113 kwa ajili ya kununua tishari
mbili zenye uwezo wa kujiendesha zenyewe (self propelled) "
“Nataka maelezo ni kwa nini mlizinunua tangu mwaka 2011 lakini zimekaa bila kufanya kazi hadi Novemba mwaka jana? Na kwa nini mnaendelea kutumia hela ya Serikali kwa kukodisha tishali kutoka Mombasa badala ya kutengeneza za kwenu au kufundisha vijana wa Kitanzania? Kwani tunao wahitimu wangapi wa fani hii?" alihoji Waziri Mkuu.
"Taarifa nilizonazo ni kwamba moja ya tishali lilidondoka baharini mkaenda kutafuta huko na kulivuta hadi hapa ndiyo maana yameshindwa kufanya kazi inavyotakiwa," aliongeza.

Katika majibu yake, Bw. Arika alisema wao waliagiza tishali
hizo kupitia ofisi ya Bandari makao makuu ambayo iko Dar es Salaam. "Pia
wakati zinaagizwa sikuwepo hapa Tanga. Nimekuja mwishoni mwa mwaka jana,"
alisema Mkuu huyo wa Bandari ambaye inaelezwa alitokea Mamlaka ya Bandari Dar
es Salaam.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alimtaka Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Bibi Mwantumu Mahiza awaite watu wa Mamlaka ya Mapato (TRA), Mamlaka ya
Bandari na Jeshi la Polisi wakae na kutafuta mbinu za kudhibiti njia za panya
zinazotumika kupitisha sukari ya magendo.
"Mkuu wa Mkoa simamia hawa watu, msaidiane kudhibiti uingizaji wa sukari kwa njia za panya. Kuna majahazi yanaleta sukari kutoka Brazil. Mheshimiwa Rais amepiga marufuku uingizaji wa sukari kutoka nje ili viwanda vyetu vya ndani viweze kuongeza uzalishaji. Dhibitini bandari zote ndogondogo hadi Pangani," alisema Waziri Mkuu.

Alisema changamoto inayoikabili Serikali ni kwamba hata
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) au Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)
hawawezi kuzikagua sukari hizo na hazijulikani ubora wake licha ya kuwa
zinafika kwa walaji.
Waziri Mkuu amerejea jijini Dar es salaam leo jioni.
0 comments:
Post a Comment