Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imetiliana saini hati ya makubalino na
taaisi ya Good Neighbour Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa skuli ya sekondari na
kituo cha utangazaji wa redio na televisheni.
Skuli
hiyo itakayokuwa na madarasa 12 itajengwa
huko kwarara wilaya ya Magharibi B kwa ushirikiano kwa ushirikiano na taasisi
mbalimbali za korea ikiwemo shirika la utangazaji la nchi hiyo SBC, kampuni ya
uhandisi na Shirika la maendeleo la Korea KOICA litakalotoa zaidi ya shilingi
bilioni 2.1 za kitanzania.
Akizungumza
baada ya utiaji saini huo katibu mkuu wizara hiyo Khadija Bakari Juma amesema mradi
huo utapunguza matatizo ya wanafunzi wa eneo hilo kufuata skuli masafa ya mbali
hali itakayoondosha wasiwasi kwa wazazi.
“Kwa
kweli hii ni faraja kubwa kwa wanafunzi
eneo hili la kwarara lilokosa skuli kwa muda mrefu wanaolazimika kuenda hadi fuoni au maeneo mengine ya mbali ili
kufuata masomo” amesema.
Katibu
mkuu amelishikuru shirika hilo kwa kufanikisha mradi huo utakaonza hivi karibuni na kituo
chake pia utafanikisha kutumia kuandaa vipindi vya kutoa elimu kwa uhakika huku
pia akiahidi wizara hiyo itaiisaidia kupata masamaha wa kodi wa vifaa mbalimbali
itakavyotumiwa katika ujenzi huo.
Nae
mwakilishi mkaazi wa taasisi ya Good Neighbor ya Tanzania Namun Heo amesema
wataweka vifaa vyote vya utangazaji nadani ya studio ya skuli hiyo pamoja na
kutoa mafunzo kwa watendaji nchini Korea na wengie watakuja Zanzibar kufundisha
Amesema
pia ndani ya kituo hicho cha matangazo lengo ni kuandaa pia vipindi mbalimbali vya
kutoa elimu kwa jamii ikiwemo haki za wanawake watoto na masuala mengine muhimu katika maisha ya kila siku.
0 comments:
Post a Comment