January 26, 2016

Jeshi la polisi Mkoa wa Kusini Unguja limesema hoteli ya  kitalii ya Konokono iliyopo Michanvi  Mkoani humo imeungua kutokana na moto uliokuwa ukiwashwa  karibu na hoteli hiyo.
Hoteli hiyo iliyoungua jana majira ya saa 5:30 inamilikiwa kwa pamoja na Bi Amina Amani Abedi Karume na ria wawili wa Italia Andrea Chiapo na Luca Gambilura  ambapo nyumba tatu na mgahawa mmoja iliungua na kusababisha  hasara ya shilingi milioni mia nne.
Kamanda wa polisi Mkoa huo Juma Sadi Khamis amewaambia waandishi wa habari kuwa upelezi umeonesha kuwa moto  huo uliwashwa na watu waliokuwa wakisafisha  eneo la kiwanja karibu na hoteli hiyo na cheche zake ziliruka kufuatia upepo mkali na kuleta madhara hayo.
“Mimi naona tusiwe tunakuza mambo sisi tumegundua hivyo wala si kweli hoteli hiyo haijachomwa kwa  sababu za kisiasa kama inavyodaiwa na baadhi ya watu”. amefafanua Kamanda Sadi.
Ameongeza kuwa tayari watu wawili waliokuwa wakisafisha eneo hilo wanaendelea kushikiliwa na jeshi hilo kwa uchunguzi zaidi.

Kamanda Sadi amefahamisha kuwa si busara watu kutoa taarifa bila ya uchunguzi kwani matukio ya kuungua moto kwa aina hiyo  katika kipindi cha kiangazi yanatokea mara kwa mara abapo hivi karibuni hoteli nyengine ya Mnana iliyopo kizimkazi na nyumba moja iliungua huko Dunga.

0 comments:

Post a Comment