January 27, 2016

Jumla ya tani 4,711 za karafuu kavu zenye thamani ya shilingi  bilioni 66 zimenunuliwa na Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar ( ZSTC)  kisiwani  Pemba, tangu kuanza kwa msimu wa karafuu hadi kufikia mwanzoni mwa mwezi huu wa January.
Afisa mdhamini wa ZSTC Abdalla Ali Ussi, amesema shirika hilo limejipanga kununuwa karafuu zote bila ya kumkopa wakulima hata mmoja sambamba na kuwalipa fidia wachumaji wa zao hilo watakaopata hasara ya kuanguka mikarafuu kwa bahati mbaya.

Nae Mkurugenzi fedha wa shirika hilo Ismail Khamis Bhai amesema kwa mwaka 2015/2016  limetowa mkopo  kwa wakulima wa karufuu Zanzibar wa zaidi  ya shilingi milioni 342.

0 comments:

Post a Comment