Wananchi wa Tanzania watahadharishwa juu ya
ugojwa wa homa ya Zika uliripotiwa kutokea katika nchi za Amerika ya
kusini hivi karibuni.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mijini Dodoma na Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee Mhe. Ummy Mwalimu alipokuwa akitoa tamko juu ya uvumi ulioenea kuhusu homa ya Zika iliyoenea katika nchi za Amerika ya kusini. Mhe.Ummy Mwalimu amewaasa watanzania kuwa na tabia ya kwenda hospitali kila wanapojisikia dalili za homa na kupima kwani sio kila homa ni malaria kwani dalili za homa ya malaria zinafanana kabisa na dalili za ugonjwa wa homa ya Zika.

“ Nawaomba ndugu zangu watanzania tuzingatie
usafi ili kuzuia mazalia ya mbu kwani ugonjwa huu unatokana na virusi
vinavyoenezwa na mbu na hao mbu wanapatikana sana nyakati za asubuhi mchana na
jioni hivyo nawasihi kutumia dawa za kuua mbua na vyandarua wakati wa kulala.”
“Napenda kutoa tamko kuwa ugonjwa huu wa homa ya Zika haujaingia Tanzania na tunawaomba watanzania kuwa makini sana na waripoti dalili zozote ambazo sio za kawaida zitakazojitokeza na mpaka jana kwa taarifa tulizonazo hakuna mgonjwa aliyegundulika kuwa na homa ya Zika” alisema Mhe.Mwalimu.

Aidha naye Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali
ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu Chaula amesema wamejiandaa kukabiliana na kesi
zozote zinatazojitokeza za homa ya Zika na wana mfumo mzuri wa kubaini magonjwa
ya mlipuko na pia kuna maabara ya NIMR ambayo inafanya uchunguzi juu
ya magonjwa mbalimbali.
“ Nawaomba watanzania kutopuuzia dalili zozote
za homa na kuamua kujitibia manyumbani au kunywa dawa bila kupima na kujua hiyo
homa ni ugonjwa gani kwani yaweza kuwa homa ya Zika” Alisema Dkt Chaula.
Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee wa kushirikiana na Shirika la Afya Dunianoi (WHO) wanafatilia kuhusu ugonjwa huu na watatoa maelekezo ya kuzingatia ili kuzuia kuenea kwa ugonjwa huu ila mpaka sasa ugomjwa huu haujaingia Tanzania.

Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii, Watoto na
Wazee Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Waandishi wa Habari Mijini Dodoma
(Hawapo Pichani) akitoa tamko la Wizara juu ya ugonjwa wa homa ya
Zika kushoto ni Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Dodoma Dkt Zainabu
Chaula.
Maelezo
DSM
0 comments:
Post a Comment