January 31, 2016

Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amesema kuwa miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM ni kilele tosha cha kupatikana kwa maendeleo katika Nyanja mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kisiasa.
Amesema kuwa maendeleo yaliyopatikana katika serikali zote mbili ya Tanzania bara na Zanzibar yamesimamiwa na miongozo, ilana na mikakati mbali mbali iliyotokana na CCM.
Alikuwa akizungumza katika uziunduzi wa miaka 39 ya kuzaliwa kwa chama hicho katika viwanja vya Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar,
Dkt. Shein amesema kuwa CCM iliyozaliwa mwaka 1977 baada ya kuungana kwa vyama viwili vya ukombozi vikiwemo TANU na Afro shraz party (ASP), chama hicho kimeweza kupigania haki za wanyonge kwa kusimasmisha serikali zenye misingi imara ya kuwatumikia wananchi kwa moyo wote bila ya ubaguzi.
 “ Serikali nyingi zilizoundwa na vyama vya ukombozi duniani zimeangushwa na wakoloni kwa njia za kiutapeli lakini sisi serikali zetu bado ni imara na zitaendelea kutawala wananchi kwa njia bora na za kidemokrasia….
Pia ni lazima tuendelee kujitathimini kwa kila jambo nje na ndani ya chama chetu kwani bado kuna changamoto mbali mbali zinazotakiwa kufanyiwa kazi ipasavyo”, amesema Dkt. Shein.
Aidha amewasihi wafuasi wa chama hicho na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu, ili wapoatikane viongozi wa kuongoza dola kwa mniaka mitano ijayo.
Dkt Shein amewataka wananchi kuendelea kulinda Amani na utulivu wa nchi na kuepuka kutumiwa na baadhi ya vyama vya kisiasa kufanya vurugu sizisokuwa na msingi kwa maslahi ya nchi.
Amefafanua kuwa msingi wa uchaguzi wa marudio upo kikatiba kwani uchaguzi mkuu uliopita ulifutwa kisheria na mamlaka iliyokuwa inahusika na usimamizi na uratibu wa uchaguzi huo baada ya kubaini kasoro.
Akizungumzia mgogoro wa kisiasa uliopo Zanzibar, Dkt. Shein amesema kuwa ulikuwa utatuliwe kwa njia za mazungumzo lakini kiongozi wa CUF ambaye ni Maalim  Seif Sharif Hamad aliyeomba mazungumzo ya maridhiano kabla hayajamaliza alienda  kutoa siri za vikao kwa waandishi wa habari Dar es saalam  na baadae kuandika barua ya kujitoa katika mazungumzo hayo.
Aidha amewataka wananchi kuendelea kulinda Amani na utulivu wa nchi na kuepuka kutumiwa na baadhi ya vyama vya kisiasa kufanya vurugu sizisokuwa na msingi kwa maslahi ya nchi.
Akizungumza katika hafla hiyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai amesema kuwa Zanzibar CCM itaendelea kuwa chama cha wananchi wote kinachoongozwa na uzalendo.

Amesema kuwa mpaka sasa CCM Zanzibar imejiandaa kwa kila hatua katika kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio utakaofanyika Machi 20 mwaka huu.
Makamo Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula akisalimiana
na Katibu Mkuu wa CCM Taifa wakati alipowasili katika uwanja
wa Ofisi ya CCM Kisiwandui katika mkutano wa hadhara wa
uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia
 Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein
akiwasalimia  Wanachama cha Mapinduzi katika mkutano wa hadhara
wa Mikoa minne  ya Unguja mara alipowasili katika shamra shamra za
 Uzinduzi wa sherehe za miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM
katika uwanja wa Ofisi kuu 









Ally Ndota, Zanzibar

0 comments:

Post a Comment