Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein ameteua Chimbeni Kheri kuwa Mshauri wa Rais katika
masuala ya utamaduni, Juma Hassan Juma Reli
ameteuliwa kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya Zanzibar na Mdungi Makame Mdungi anakuwa Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi
na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya
Mzee Rais Shein pia amemteuwa Kai Bashir Mbarouk kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara
ya Katiba na Sheria na Noah Said kuwa Mkurugenzi
wa uendeshaji na Utumishi katika Wizara ya Kilimo na Maliasili.
0 comments:
Post a Comment