TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
1.0 Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)
1.1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli, ametengua uteuzi wa Bwana Dickson E. MAIMU,
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuanzia leo, tarehe 25
Januari, 2016.
1.2 Aidha, baada ya utenguzi huo, Bwana Dickson E. MAIMUamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao:
1.2.1 Bwana Joseph MAKANI,
Mkurugenzi wa TEHAMA
1.2.2. Bi Rahel MAPANDE, Afisa Ugavi
Mkuu
1.2.3 Bi Sabrina NYONI,
Mkurugenzi wa Sheria
1.2.4 Bwana George NTALIMA,
Afisa usafirishaji
1.3 Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa
imetumia Sh.179.6 bilioni. Kiasi hiki ni kikubwa na Rais angependa ufanyike
uchunguzi na ukaguzi jinsi fedha hizi zilivyotumika, maana Rais amekuwa
akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa
Vitambulisho vya Taifa.
1.4 Hivyo, Rais ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya
Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.
1.5 Rais pia ameelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali afanye ukaguzi maalum wa hesabu za NIDA, ikiwemo ukaguzi wa “value
for money” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa
hadi sasa.
1.6 Rais vile vile ameelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.
2.0 Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki
na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa
2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi
Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini
Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo
rafiki.
2.2 Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na
Ushirikiano wa Kianda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi
wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi
kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni:
2.2.1 Bi Batilda Salha BURIANI,
aliyeko Tokyo, Japan
2. 2.2 Dkt. James Alex MSEKELA,
aliyeko Rome, Italia.
2.3 Rais amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko
London, Uingereza, Bwana Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya
Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa
atakapopangiwa kazi nyingine.
2.4 Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko
wazi:
2.4.1 London, kufuatia kurejea nchini kwa Balozi
Peter A. KALLAGHE
2.4.2 Brussels, kufuatia aliyekuwa Balozi,
Dkt. Deodorous KAMALAkuchaguliwa kuwa Mbunge.
2.4.3 Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa
mkataba wa Dkt. James Alex MSEKELA.
2.4.4 Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa
mkataba wa Bibi Batilda BURIANI
2.4.5 Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia
aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz Ponray MLIMA, kuteuliwa kuwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa
Kikanda na Kimataifa.
2.4.6 Brasilia, Brazil, kufuatia kustaafu
kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis MALAMBUGI.
3.0 Tawala za Mikoa
3.1 Rais ametengua uteuzi wa Eng. Madeni Juma KIPANDE kabla
hajathibitishwa kwenye cheo cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na
utendaji kazi usioridhisha.
4.0 Utumishi
wa Umma
3.2 Nachukua nafasi hii kuwahimiza viongozi wote katika Utumishi
wa Umma, na watumishi wote wa umma, kubadilika kwa dhati kwenye utendaji wao na
uadilifu wao.
3.3 Napenda kusisitiza kuwa Rais na sisi tunaomsaidia hatuoni
raha kuchukua hatua dhidi ya viongozi na watumishi wengine. Tungependa kila mtu
mwenyewe ajirekebishe na kutomfikisha Rais mahali ambapo inabidi amchukulie
hatua.
Mambo yafuatayo ni muhimu:
Mambo yafuatayo ni muhimu:
4.2.1 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu isipate
kigugumizi kusimamia utendaji na maadili ya kazi.
4.2.2 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu asipate
kigugumizi kuchukua hatua za nidhamu, lakini afanye hivyo kwa kuzingatia kwa
ukamilifu sheria, kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma.
4.2.3 Lazima uongozi na watumishi wa umma
wawahudumie wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima. Kwa sababu hiyo:
a) Kila ofisi ya Serikali iwe na dawati la kusikiliza
shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
b) Kwenye kila Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa
Wilaya wajenge uwezo wa kushughulikia shida za wananchi kwa ukamilifu na kwa
wakati. Kwa muundo wa Serikali yetu hakuna sababu kwa mwananchi kufunga safari
mpaka Ikulu Dar es Salaam kwa kuamini kuwa ni Rais tu anayeweza kumaliza
matatizo yake, maana wawakilishi wa Rais wako kila pembe ya nchi yetu. Ikibidi
wananchi wafike Ikulu ina maana hao wawakilishi wa Rais hawakutimiza wajibu
wao.
c) Kuanzia sasa watumishi wote wa umma wavae majina
yao ili iwe rahisi kwa mwananchi kumtambua anayemhudumia na hivyo kumsifu
mtumishi wa umma anayewahudumia kwa weledi, uaminifu na kwa wakati, na kumtolea
taarifa yule anayefanya mambo ya hovyo.
d) Kila ofisi ya Serikali iwe na utaratibu wa kupokea maoni
ya wananchi kuhusu huduma inayotolewa kwenye ofisi hizo, na kushughulikia
haraka maeneo yote ambayo wananchi wataonesha kutoridhika na huduma.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Arusha
25 Januari, 2016
0 comments:
Post a Comment