January 11, 2016

Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hamad Yussuf Masauni ameitaka idara ya uhamiaji Zanzibar kushughulikia wahamiaji wanaoishi nchini kinyume cha sheria.
Amesema watu hao baadhi yao ndio wanaojihusisha na  vitendo vya uhalifu nchini hivyo lazima kuchunguzwa ili kufuata taratibu ziliopo ikiwa ni hatau ya kulinda usalama wa Tanzania.
Akizungumza maafisa wa idara ya Uhamiaji Zanzibar  alipoitembelea idara hiyo Masauni amesema ingawa wageni wanaokuja Tanzania wanachangia pato la taifa, lakini ni lazima wafuate taratibu zilizowekwa kisheria.
Amefahamisha kuwa zoezi hilo linaloendeea la kupambana na wahamiaji haramu wanaoishi Tanzania na kufanya kazi kinyume cha sheria linatekelezwa kwa mujibu wa sheria na kuwataka wananchi kuacha upotoshwaji kuwa kuwa raia hao wa kigeni wanafukuzwa bila ya kufuatwa taratibu.
Naibu waziri Masauni pia ameitaka idara hiyo ya uhamiaji Zanzibar  kushughulikia na kufanya uchuguzi wa kina juu ya kutolewa hati za kusafiria kiholela ili kuchukuliwa hatua kwa wahusika.
Aidha amewataka watendaji hao kujitathimini kiutendaji ilikwenda kasi na utendaji wa serikali na kuhakikisha kila siku ya alhamisi wanawasilisha  ripoti katika makao makuu ya uhamiaji lengo likiwa ni kujua utekelezaji wa majukumu yao kwa kila wiki,

Kwa uapnde wake  Naibu Kamishna utawala wa fedha idara ya Uhamiaji Zanzibar George Cheko Kaswede amesema malalamiko mengi yanayotolewa dhidi ya ucheleweshaji wa hati za kusafiria Zanzibar  yanasababishwa na waombaji kuchelewa kutimiza masharti yanayohitajika.


0 comments:

Post a Comment