January 11, 2016

Makamu wa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inafanya kazi kubwa katika kuwasaidia wajasiriamali wadogo ili kujiendeleza kiuchumi.
Amesema makakati huo unaenda sambamba na dhana ya uwezeshaji wananachi kiuchumi ikiwa ni lengo la kupambana na umasikini Zanzibar.
Akizungumza katika ufunguzi wa kituo cha kukuza na kulea wajasiriamali huko Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar amesema kufanya hivyo pia kutawawezesha vijana ambayo ni nguvu kazi kujikwamua na tatizo la ajira nchini.
Makamo wa  rais Samia amesema kituo hicho cha ujasiriamali kimekusudia kukuza ubunifu kwa vijana itakayotumika katika kujenga taifa.
Amewataka vijana waliobahatiaka kuchaguliwa kujiunga na kituo hicho kuitumia fursa hiyo ili kujiajiri wenyewe pamoja kuwasaidia vijana wengine.

Katibu mkuu Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa jamii vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Asha Ali Abdallah amesema kituo hicho cha ujasiriamali kilichozinduliwa kinakusudia kutoa taaluma za ujasiriamali, biashara na utalii na elimu ya teknolojia ya habari na mawasiliano.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo kutoka kwa Time Mohammed juu ya utenganishaji wa maji na maziwa
katika kituo cha kukuza na kulea wajasiriamali (ZANZIBAR TECHNOLOGY
AND BUSSNESS INCBATTION CENTER-ZTIBI)  kiliopo Mbweni
nje kidogo ya mji wa Zanzibar ikiwa ni moja ya miongoni mwa  
shamra shamra  ya kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi Zanzibar
 inayofikia kilele chake kesho.

0 comments:

Post a Comment