JUMLA
ya kesi 106 za makosa ya usalama barabani zimekamatwa kufuatia operesheni maalum
iliyofanywa na Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Unguja.
Kesi
hizo zimehusisha vyombo mbalimbali vinavyotumia barabara ikiwemo vespa, gari za
abiria ambazo zimewekwa tinted uchakavu wa vyombo pamoja na kumalizika kwa bima
na leseni za njia.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kusini Juma Saadi Khamis, amesema katika operesheni hiyo
wameamua kuanza kutoa hukumu ya papo kwa papo kwa wanaokutwa na makosa ya aina
hiyo.
Amfahamisha
kuwa katika wiki iliyopita jumla ya
vyombo 75 walishitakiwa na jumla ya faini ya shilingi 2,526,000/= zilipatikana.
Amesema
kuwa hivi sasa operesheni hizo za kikosi cha usalama barabarani ni endelevu ili
kuzuwia makosa ya barabarani. Amewashauri madereva wanaoendesha vyombo vya moto
kuwa waangalifu wanapokuwa barabarani, sambamba na kuvipasisha vyombo vyao ili
kuweza kuepuka makosa yasiyokuwa ya lazima.
Hata
hivyo Kamanda Saadi amesema kuwa malengo ya Mkoa huo ni kudhibiti ongezeko la
makosa ya usalama barabarani na kupunguza ajali zisizokuwa za lazima, sambamba
na kutoa elimu kwa wadau dhidi ya matumizi sahihi ya barabara.
Akizungumzia
ulinzi wa mkoa wa Kusini kamanda Saadi amesema wameijipanga kuwadhibiti wahalifu wakubwa na baadhi ya watu
wanaojihusisha na uvunjifu wa amani
na usalama kwa watu na mali zao mkoani
humo.
0 comments:
Post a Comment