Jumla ya eka tisa (9) za
mashamba ya mikarafuu imechomwa moto na watu wasiojulikana na kusababisha
hasara kuwa kwa wamiliki ya mashamba hayo katika bonde la Mkanyageni Shehia ya
Mzambarauni Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Moto huo ulilotokea Janauri 22 mwaka huu umeathiri
zaidi ya mikarafuu 151 katika mashamba hayo.
Akizungumza katika eneo la tukio Mkuu wa Wilaya
ya Wete Rashid Khadidi Rashid amesema kitendo cha kuchoma moto
mashamba hayo ni kuhujumu uchumi wa nchi pamoja na wananchi wake na serikali
itahakikisha inawasaka na kuwakamata wahusika ili kufikishwa mahakamani .
Amefahamisha
kuwa kuchomwa moto mashamba hayo ni hujuma za makusudi zilizofanyika ,
kwani moto huo umetokea katika maeneo na mashamba tofauti.
“Serikali haiwezi kuvifumbia macho vitendo vya
kuhujumu uchumi wake, hivyo naviomba vyombo vya sheria kufanya uchunguzi wa
kina ili wahusika waweze kupatikana na kufikishwa mahakamani ”amesisitiza.
Mmoja wa wananchi wakaazi wa shehia
hiyo Hamad Bakari Makame akizungumza na
mwandishi wa habari hizi amesema kitendo hicho kimesababisha athari
kubwa ya kiuchumi na kimazingira .
Amefahamisha kuwa mkarafuu mmoja unauwezo wa
kuzalisha zaidi ya pishi ishirini ambazo kwa sasa ni sawa na zaidi ya shilingi
laki nne.
0 comments:
Post a Comment