December 03, 2015



Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Tanzania inatarajia kuendesha zoezi la ugawaji wa dawa kwa ajili ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele.

Zoezi hilo linatarajiwa kufanyika kwa  ushirikiano na Ofisi za mikoa mbalimbali  na dawa zitakazotolewa kwa Magonjwa ya mabusha, matende, usubi, trakoma, minyoo, kichocho  na zitatolewa bure kwa wananchi wote kuanzia umri wa miaka mitano hadi kuendelea.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Mratibu wa Kitaifa wa Mpango wa Taifa wa kudhibiti magonjwa  Dkt. Upendo Mwingira  alipokuwa akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari mbalimbali nchini.
Dkt. Mwingira amesema kuwa dawa  hizo zitatolewa kwenye Hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati Masoko, Vituo vya Basi, treni , katika skuli, mashirika ya umma, nyumba za ibada, kambi za jeshi na katika mawizara.
Dkt. Mwingira amesema kampeni hiyo itaanza katika jiji la Dar es Salaam mwezi huu na katika mikoa mengine ni Katavi, Rukwa, Lindi, Mtwara, Singida, Dodoma na Pwani.
Ameeleza kuwa katika Mikoa iliyobakia kampeni hiyo itafanyika kwa awamu kati ya Januari na Februari mwaka huu na dawa zitakazotolewa hazina madhara yoyote. 




MAELEZO-Dar es salaam

0 comments:

Post a Comment