Serikali ya Tanzani kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais imesema inaanzisha utaratibu wa
kuendesha vikao kazi kwa kutumia
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano TEHEMA.
Mfumo huo utawezesha kikao kimoja
kuunganisha washiriki kutoka mikoa nane na wajumbe wake kuwasiliana
moja kwa moja kwa maswali na ufafanuzi.
Mkuu
wa Kitengo cho Mawasiliano Serikalini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti
ya Utumishi wa Umma, Florence Temba amesema kuanzia sasa Serikali haitagharamia gharama zozote za
kuendesha vikao kazi na watendaji wake badala yake vitaendeshwa Teknolojia hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam amesema kuwa kupitia utaratibu huo
washiriki wa vikao hivyo hasa Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa
Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa watabaki katika maeneo ya kazi na wataunganishwa
na mtandao huo.
“
Awali ilitakiwa lazima watumishi
wasafili kuja Dar es Salaam kwa ajili ya mkutano lakini kwa sasa tutatumia
Video Conference iliyounganishwa kwenye mikoa yote nchini. tutaokoa gharama za
nauli, mafuta, chakula na malazi,” amesema Temba.
Mfumo huo Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
TEHEMA umeanzishwa na Serikali mwaka 2013/2014 katika mikoa ya Kilimanjaro,
Kagera, Morogoro na Iringa kati ya utumishi na mamlaka za Serikali za mitaa na sasa
yanapatikana nchi nzima isipokuwa mikoa mipya ya Geita, Simiyu, Katavi na
Njombe.
0 comments:
Post a Comment