JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
KURUGENZI
YA MAWASILIANO YA RAIS, IKULU
Simu: 255-22-2114512,
2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Faksi: 255-22-2113425
|
|
OFISI
YA RAIS,
IKULU,
1 BARABARA YA BARACK OBAMA,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO
VYA HABARI
Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa
kadi za Christmas na Mwaka Mpya kwa gharama za serikali/umma, kwa mwaka huu.
Balozi Sefue,
ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo, afanye
hivyo kwa gharama zake mwenyewe.
Badala yake Balozi
Sefue ameagiza fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji na uchapishaji wa
kadi, zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, Idara na Taasisi za umma
zinadaiwa na wananch/wazabuni waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe
katika matumizi mengine ya kipaumbele.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
26 Novemba,
2015
0 comments:
Post a Comment