May 09, 2014


 Wauguzi wa Zanzibar wameanza kuadhimisha siku ya waaguzi Duniani huku wakielezea kuwa bado wanakabiliwa na matatizo kadhaa yanayohitaji kupatiwa ufumbuzi ili huduma bora za wagonjwa kuimarika.
Maadhimisho yatafikiwa kilele chake siku ya tarehe 12 mwezi huu yameanza kuadhimishwa Wilaya ya Wete kwa mkutano wa hadhara katika Shehia ya Ole .

Mkuu wa kitengo cha Wauguzi cha Hospitali ya Wete Dk Sabra Salim Suleiman akizungumza na wananchi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani amesema moja ya matatizo hayo ni pamoja na upungufu wa vitendea kazi .

hata hivyo ametoa wito kwa Wauguzi waliopo kufuata maadili ya kazi zao ikiwa ni pamoja na kutotumia lugha mbaya kwa wagonjwa.   
"iwapo wauguzi watatekeleza vyema wajibu wa kazi zao kwa kijiepusha maneno machafu kwa wagonjwa , watathaminiwa na jamii inayowazunguka". amesema Dk Sabra.

0 comments:

Post a Comment