May 12, 2014

Shirika la taifa la biashara Zanzibar ZSTC   imevuka lengo na kununua ya tani 5345za za karafuu  iliyokusudia kununua tani 3400 kwa mwaka 2013/2014.
Mkurugenzi muwezeshaji   ZSTC Pemba Mwanahija Almasi Ali amesema mbali ya mafanikio hayo  bado kuna changamoto kwa baadhi ya wakulima  kuchanganya  matende na makonyo na  kuharibu sifa  na ubora wa zao  hilo katika soko la dunia.
Akizungumza na wadau wa zao la karafuu kwa wilaya ya Micheweni amesema ZSTC imevuka lengo hilo kunatokana na wakulima kufuata taratibu za shirika hilo.
Wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa Musini Pemba Juma Kassim Tindwa amewataka wakulima na wananchi kuendelea na vita vya kukomesha magendo ya karafuu kwa faida ya wakulima na taifa.
Akizungumza katika mkutano huo wa wadau wa zao la karafuu wa wilaya ya chake amesisitiza wazanzibar kuongeza uzalishaji  wa zao hilo pamoja na kurejesha ubora unaohitajika katika soko la dunia.

0 comments:

Post a Comment