May 15, 2014

 Mamlaka ya uhifadhi ya mji Mkongwe Zanzibar imekamilisha michoro ya ujenzi wa sehemu za kusubiria watu wenye wagonjwa katika hospitali kuu ya mnazi mmoja.
Michoro hiyo imeandaliwa baada ujenzi wa awali kuzuiliwa kutokana na kutishia kuharibu haiba yake  hali halisi ya uhifadhi wa mji huo wa kihistoria.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Issa Sariboko Makarani amesema ujenzi wa eneo hilo hautakuwa wa kudumu kwa vile eneo hilo la mbele ya hospitali hiyo nila bustani ya kihistoria na lipo karibu na ikulu rais wa Zanzibar.
Kw amujibu wa mchoro huo sehemu hiyo itakapokamilika itakuwa na uwezo wa  kutumiwa na kiasi cha watu mia nne hali itakayopunguza msongamano wa katika maeneo ya hospitali.
 Hospitali ya mnazi mmoja iliomba kujenga sehemu hiyo kwa ajili ya kupata sehemu ya kusubiria watu wenye wagonjwa ambayo kwa sasa ni moja ya tatizo kubwa linaloikabili  hali inayosababisha msongamano mkubwa.

0 comments:

Post a Comment