Afisa wa Wizara ya Uwezeshaji Ustawi wa jamii Maendeleo ya Wanawake na Watoto Halima Masheko ameitaka jamii kuthamini malezi ya pamoja ili kudhibiti ongezeko la vitendo vya udhalilishaji kwa watoto.
Amesema ni vyema kuweka mikakati ya pamoja katika kulinda watoto kwani anapokutwa na vitendo hivyo jamii ndio inayoathirika.
Amefahamisha kuwa ni lazima ieleweke kuwa mbali na elimu inayotolewa bado jamii imekuwa inamaliza kesi hizo kwa njia ya mazungumzo hali inayochangia kukua kwa tatizo hilo.
Hivyo amehimiza Afisa Halima amesisitiza kuchukuliwa juhudi na ushirikiano katika kupambana katika kutetea maslahi ya watoto ili kuwa na jamii salama na vitendo hivyo vya udhalilishaji.
0 comments:
Post a Comment