April 18, 2014

Wizara ya Fedha imetangaza kufuta malipo ya Wabunge waliosusia vikao vya mchakato wa Katiba vinavyoendelea Dodoma.
Uamuzi huu umetangazwa ikiwa ni siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka matusi na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Taarifa hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba, na kuziagiza Benki zote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance ambazo zilipelekwa Bungeni April 16 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka April 30

0 comments:

Post a Comment