April 18, 2014

Wavuvi katika Ghuba ya Minai wametakiwa kuendelea na shughuli zao za uvuvi na  kuacha kutegemea mapato yatokanayo na michezo inayofanywa na watalii katika Ghuba hiyo.Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya uvuvi Mussa Aboud Jumbe amesema kumeibuka shughuli za utalii  katika ukanda huo kwa kurusha vishada hali inayonyesha wavuvi kujisahau juu ya mazingira ya bahari kutokana na ruzuku wanayopewa.
Akizungumza na wavuvi wa Ghuba ya Minai huko Mkoa wa kusini Unguja  Amewataka wavuvi hao kurejea na shughuli zao uvuvi kwa vile ni njia tegemeo ya kupata pato la uhakika.
Amesema urushaji wa vishada unaweza kuleta athari katika mazingira na kusababisha  kutoweka samaki kutokana na mshindo unaotokea wakati vinapoanguka katika bahari.
Nao wavuvi hao wameahidi kukaa pamoja kupanga mikakati itakayowasaidia katika shughuli za uvuvi pamoja na watalii hao.
 

0 comments:

Post a Comment