Jeshi la Polisi Zanzibar
limesitisha mkutano wa hadhara wa chama
cha CUF uliopangwa kufanyika leo katika viwanja vya demokrasia Kibandamaiti.
Taarifa iliyotiwa saini na Mkuu
wa polisi Wilaya ya Magharibi SSP Ramadhan Nganga imeleza kuwa mkutano huo
umesitishwa kwa sababu za kiusalama.
Amemtaka katibu mkuu wa CUF
kuwajuilisha wanachama na wapenzi wote chama hicho kuwa watulivu kwa muda huo
hadi hali itakaporuhusu kufanyika tena kwa mkutano huo.
Mkutano huo wa CUF ulitarajiwa
kuwahusisha wajumbe wa bunge maalum la katiba kutoka umoja wa katiba ya
wananchi ukawa waliosusia vikao vya
bunge hilo linaloendelea mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment