Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi
Seif Ali Idd ameelezea masikitiko yake kufuatia kitendo cha baadhi ya wajumbe wa bunge maalum la Katiba
kususia vikao vya bunge hilo.
Amesema wabunge hao hawakuonyesha
uungwana wala uvumilivu na muelekeo wa
kuwanyima haki ya kidemokrasia watanzania.
Hata hivyo ameeleza kuwa kundi
lililobakia ndani ya bunge hilo kwa mujibu wa sheria na kanuni lina uwezo wa
kuendelea na kazi ya kuandaa katiba na baadaye kuipeleka kwa wananchi kupigiwa
kura ya maoni.
Kundi lililobakia ndani ya Bunge
Maalum la Katiba ni kubwa na lina uwezo wa kutekeleza kazi hiyo muhimu katika
Historia ya Tanzania kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zetu tulizojipangia kwa
pamoja sisi na wale walioamua kuukimbia mjadala huo “. Alifafanua Balozi
Seif.
Balozi seif akizungumzia suala la
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar amesema umeleta faida kubwa ikiwemo
kuwanufaisha watanzania wengi kiuchumi na ustawi wa jamii.
Amebainisha kuwa Kwa vile
Muungano wa Wananchi wa Zanzibar na Tanzania Bara ni wa asili ni vyema kwa watu
wa pande hizo mbili wakaendelea kuuenzi na kuuimarisha kwa faida ya vizazi vya
sasa na vile vijavyo.
Makamu wa pili
wa Rais Zanzibar ameeleza hayo alipotembelea maonyesho ya maadhimisho ya
kutimia miaka 50 ya muungano katika viwanja vya mnazi mmoja jijini dar es
salaam yaliyozirishirikisha mashirika na taasisi mbali mbali za sekta za
Muungano.
Add caption |
Balozi Seif akipezuri na
kuangalia baadhi ya Machapisho yaliyoandikwa katika Gazeti Rasmi la Serikali
kuhusu harakati za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kati kati ya miaka
ya Sitini.
|
0 comments:
Post a Comment