Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif
Sharif Hamad, amesema waislamu wa Zanzibar na tanzania kwa ujumla wamepata pigo
kwa kuungua studio za Radio Noor FM hivi karibuni.
Makamu wa Kwanza wa
Rais Maalim. Seif Sharif Hamad akisalimiana na Aboubakar Fakih Mtangazaji wa Radio Noor FM katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar |
Akitembelea studio hizo katika jengo la msikiti wa Masjid Sahaba Mtoni Kidatu ziliozungua tarehe 09 mwezi huu amefahamisha kuwa kituo hicho ni muhimu na kimesaida kutoa taaluma mbali mbali zikiwemo zile zinazohusiana na maadili ya kiislamu jambo linalosaidia serikali katika kurejesha maadili mema kwa jamii.
Maalim Seif amesema wananchi wanajifunza mengi kupitia matangazo ya Radio Noor kutoka na kutoa fursa kwa masheikh na wanataaluma kusambaza taaluma kwa jamii.
Ametoa pole kwa uongozi wa Radio hiyo kutoa wito kwa waislamu wenye uwezo kuichangia radio hiyo ili kurejesha matangazo yake haraka na kuahidi kuchangia shilingi milioni tano.
Nae Mkurugenzi wa Radio hiyo Sheikh Mohd Suleiman amesema tukio hilo la kuungua studio za kurushia matangazo pamoja na vitendea kazi vyake vinavyokisiwa kugharimu shilingi milioni themanini (80) na ni mfululizo wa matukio ya aina hiyo yaliyowahi kukikumba kituo hicho tangu kuanzishwa kwake miaka mitano iliyopita.
Wakati huo huo Maalim Seif amemtembelea mtangazaji wa Radio abubakar fakih katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja aliyalazwa aliyejeruhiwa miguu pamoja na mkono wake wa kulia baada ya kujitupa kutoka ghorofa ya pili kuokoa maisha yake.
Kwa mujibu wa daktari wa zamu wa hospitali hiyo dokta Said Omar, mgonjwa huyo hali yake inaendelea vizuri na atabakia hospitalini hapo kwa kipindi kisichopungua miezi miwili .
0 comments:
Post a Comment