RAIS wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema kuwa Msumbiji
na Tanzania ni nchi zenye historia katika uhusiano na ushirikiano wao hivyo
kuna haja ya kuendelezwa na kuimarishwa zaidi kwa manufaa ya pande mbili hizo.
Dk. Shein aliyasema
hayo leo wakati wa mazungumzo kati yake na Balozi mpya wa Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa
Tanzaniam Monica Patricio Clemente Mussa
aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kujitambulisha.
Katika mazungumzo
hayo, Dk. Shein alisema kuwa uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na
Msumbuji ni wa kihistoria ambao umeasisiwa na viongozi wa wa Mataifa hayo akiwemo
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Marehemu Mzee Abeid
Amani Karume na Hayati Samora Machel.
Akisisitiza juu
ya uhusiano na ushirikiano wa kidugu kati ya Zanzibar na Masumbiji, Dk. Shein
alisema kuwa katika kuliimarisha hilo Zanzibar hivi sasa kuna WanaMsumbujini
wengi wanaoishi na waliozaliwa ambao wanaishi na Wazanzibari kama ndugu.
Kutokana na
juhudi na hatua hizo, Dk. Shein alisema kuwa mashirikiano katika sekta kadhaa
za maendeleo ni muhimu na ya msingi kwani yanaweza kuleta tija na mafanikio
zaidi kwa pande zote.
Aidha, Dk. Shein
alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa mafanikio makubwa iliyoyapata Msumbiji
katika kuimarisha uchumi wake sambamba na mafanikio katika sekta nyengine za
maendeleo.
Aidha, Dk. Shein
alisema kuwa Zanzibar ikiwa ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inathamini sana uhusiano na ushirikiano huo uliopo kati ya Msumbiji na Zanzibar
na kueleza kuwa mashirikiano yanayoendelezwa yatasaidia katika uimarishwaji wa
sekta za maendeleo zikiwemo elimu, kilimo, gesi na mafuta, biashara, utalii na
nyenginezo.
Akizungumzia kwa
upande wa sekta ya elimu, Dk. Shen alisema kuwa Zanzibar imeweza kupiga hatua
katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwa na Vyuo Vikuu Vitatu hivi sasa na
kusisitiza haja kwa Msumbiji kuleta wanafunzi wake ili kuja kusoma Zanzibar
ikiwa ni pamoja na kujifunza Lugha ya Kiswahili kupitia Chuo chake Kikuu cha
Taifa cha SUZA.
Pia, Dk. Shein
akitilia mkazo sula hilo alieleza kuwa hatua hiyo itasaidia katika kubadilishana
uzoefu ambapo itawapa fursa na wanafunzi wa Zanzibar kwenda nchini humo kusoma
lugha ya Kireno kwa lengo la kuiimarisha lugha hiyo hapa nchini ambayo ina
historia kubwa katika historia ya Zanzibar na Utawala wa Kireno uliotawala hapa
Zanzibar mnamo miaka ya 1500.
Dk. Shein alitumia
fursa hiyo kumkaribisha Balozi huyo hapa nchini pamoja na kumpongeza Rais wa
Nchi hiyo Filipe Nyusi kwa mafanikio
yaliopatikana ya kiuchumi na kimaendeleo.
Nae Balozi wa
Msumbiji katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Monica Patricio Clemente Mussa, alisema kuwa
Msumbiji inajivunia uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania ikiwemo
Zanzibar ambao ni wa muda mrefu.
Katika maelezoa
yake Balozi huyo wa Msumbiji alisema kuwa
nchi hiyo hivi sasa imeqweza kupata mafanikio makubwa kwani tayari
uchumi wake unazidi kuimarika siku hadi siku.
Aidha, Balozi Mussa
alisema kuwa miongoni mwa sekta ambazo hivi sasa zinaimarika ni pamoja na sekta
ya miundombinu, kilimo, madini, gesi na mafuta huku akisisitiza kuwa uchumi wa
nchi hiyo inaendelea kukua na kuimarika.
Katika
mazungumzo yao viongozi hao pia, waligusia haja ya kukuza uhusiano na
ushirikiano katika sekta za maendeleo.