May 09, 2014


Wabunge wa bunge la Tanzania wametakiwa kufanya kazi kwa maslahi ya taifa wanalolitumikia  na si kwa mirengo ya vyama vyao vya  siasa.

Amesema kazi ya wabunge ni kuendeleza  taifa na wananchi wanaowatumikia kwa kufanya kazi kwa pamoja.

"Waheshmiwa wabunge ombi langu sisi ni watanzania tuhakikishe tunafanya kazi kwa watanzania wenzetu waliotuchagua wao hawajali tunatoka wapi hapa kazi yetu ni bunge si chama chochote tuna mwaka mmoja tu" alisisitiza Spika Makinda.

Alikuwa akiakhirisha baada ya mwenyekiti wa wa Chadema kutangaza kambi kuu ya upinzani ya bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania lilishirikisha wajumbe kutoka chama hicho pamoja na CUF,NCCR na amepongeza wabunge wa  upinzani wa bunge hilo kwa kufikia uamuzi huo.

“Niwapongeza kwa kuchukuwa uamuzi huu mazuri unaokibalika kimataifa  uliojali maslahi ya watanzania mlinshutumu wakati wa kupitisha kanuni ila mmekubuka shuka wakati kushakucha”  alieongezea zaidi Makinda.

Hii ni mara ya kwanza tangu kuzinduliwa kwa Bunge hilo la 10 baada ya Uchaguzi Mkuu uliopita wa 2010 vyama vingine nje ya Chadema ikiwemo CUF na NCCR – Mageuzi kuunda baraza kivuli la Mawaziri .

Akitangaza baraza hilo la Mbowe amesema baraza hilo limeunganisha wabunge wa vyama vya vengine vya upinzani ili kuimarisha utendaji.

“Mhe spika naomba kutangaza baraza hilo la mawaziri wa kambi ya upinzani umeamua kuunganisha wajumbe wa ukawa  ili kupambana na serikali ya tanzania inayooongozwa na chama cha mapinduzi" alieleza Mbowe.

Kauli ya mbowe ilipingwa na spika makinda kwa kueleza kuwa suala la ukawa halihitajika kuhusishwa na bunge la Tanzania .

Muungano huo wa vyama hivyo vya Chadema, CUF, NCCR  katika bunge maalum la katiba liloisha hivi karibuni baada ya  kuanzisha ukawa pia  vina nia ya kuweka mgombea mmoja wa Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.

0 comments:

Post a Comment