Wauguzi wa Zanzibar wameanza kuadhimisha siku ya waaguzi Duniani huku
wakielezea kuwa bado wanakabiliwa na matatizo kadhaa yanayohitaji kupatiwa
ufumbuzi ili huduma bora za wagonjwa kuimarika.
Maadhimisho yatafikiwa kilele chake siku
ya tarehe 12 mwezi huu yameanza kuadhimishwa Wilaya ya Wete kwa mkutano wa
hadhara katika Shehia ya Ole .
Mkuu wa
kitengo cha Wauguzi cha Hospitali ya Wete Dk Sabra Salim Suleiman akizungumza
na wananchi katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani amesema moja ya
matatizo hayo ni pamoja na upungufu wa vitendea kazi .
hata hivyo
ametoa wito kwa Wauguzi waliopo kufuata maadili ya kazi zao ikiwa ni pamoja na
kutotumia lugha mbaya kwa wagonjwa.
"iwapo
wauguzi watatekeleza vyema wajibu wa kazi zao kwa kijiepusha maneno machafu kwa
wagonjwa , watathaminiwa na jamii inayowazunguka". amesema Dk Sabra.
0 comments:
Post a Comment