August 24, 2016



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa kampuni ya ZANTEL ukiongozwa na Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom Group, Mauricio Ramos, ikulu mjini Zanzibar
Katika mazungumzo hayo rais Shein ameeleza haja kwa kampuni ya ZANTEL  kupitia  kuimarisha utoaji huduma zake ili kupata mafanikio zaidi katika ushindani wa kibiashara.
Amesema iwapo kampuni hiyo itafanikiwa katika utoaji huduma zake ndani na nje ya nchi kutasaidia kuitangaza Zanzibar kimawasiliano na kuinua uchumi wa Taifa
Dr. Shein amesema serikali ya Zanzibar itaendeleza ushirikiano wake na kampuni hiyo ambyo serikali ina hisa zake.
Nae Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom Group,  Mauricio Ramos, amesema kampuni hiyo itahakikisha ZANTEL inapata mafanikio zaidi kutokana na mikakati madhubuti iliyowekwa hasa katika kuimarisha miundombinu yake ili kutoa huduma za uhakika.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Bw,Mauricio Ramos,Mtendaji Mkuu wa kampuni ya "Millicom Group"akiwa na ujumbe wake walipofika Ikulu Mjini Unguja kwa mazungumzo leo (kushoto) Nd,Benoit Janin Mtendaji Mkuu wa Zanztel  23/08/2016.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia)
 akisalimiana na Bibi Rachel Samren Naibu Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Millicom Group
 pia Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Zanztel (katikati) Bw,Mauricio Ramos,Mtendaji Mkuu wa kampuni 
ya "Millicom Group"(wa pili kulia) na (kushoto) Nd,Benoit Janin Mtendaji Mkuu wa Zanztel  ujumbe huo ulifika Ikulu Mjini Unguja leo kwa mazungumzo na Rais leo 23/08/2016

Mkurungenzi Mtendaji wa Millicom Group Mauricio Ramos akifurahia zawadi aliyokabidhiwa na wanafanya kazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel Zanzibar baada ya kufanya ziara ya kutembelea ofisi za kampuni hiyo Zanzibar.

Mkurungenzi Mtendaji wa Millicom Group Mauricio Ramos akiwa kwenye ya pamoja na wanafanya kazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Zantel Zanzibar baada ya kufanya ziara ya kutembelea ofisi za kampuni hiyo Zanzibar.


0 comments:

Post a Comment