Shirika la taifa la biashara Zanzibar
ZSTC imevuka lengo na kununua ya tani 5345za za karafuu iliyokusudia
kununua tani 3400 kwa mwaka 2013/2014.
Mkurugenzi muwezeshaji ZSTC Pemba Mwanahija Almasi Ali amesema mbali
ya mafanikio hayo bado kuna changamoto kwa baadhi ya wakulima kuchanganya
matende na makonyo na kuharibu
sifa na ubora wa zao hilo katika
soko la dunia.
Akizungumza na wadau wa zao la
karafuu kwa wilaya ya Micheweni amesema ZSTC imevuka lengo hilo kunatokana
na wakulima kufuata taratibu za shirika hilo.
Wakati huo huo Mkuu wa mkoa wa Musini
Pemba Juma Kassim Tindwa amewataka wakulima na wananchi kuendelea na vita vya
kukomesha magendo ya karafuu kwa faida ya wakulima na taifa.
Akizungumza katika mkutano huo wa
wadau wa zao la karafuu wa wilaya ya chake amesisitiza wazanzibar kuongeza
uzalishaji wa zao hilo pamoja na kurejesha ubora unaohitajika katika soko
la dunia.
0 comments:
Post a Comment