Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia Kongamano la Kampeni ya kukomesha mauaji dhidi ya Tembo. |
Makamo wa Rais wa Tanzania Dkt.Ghalib
Bilali amesma kuwa serikali kwa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa, inafanya
mikakati mathubuti ya kukabiliana na ujangili wa wanyamapori kwa kuwabainisha
majina wale wote wanaojihusisha na biashahara haram ya pembe za ndovu.
Akifungua mkutano huo wa siku 4 kupinga
ujangili dhidi ya tembo uliongezeka mbali na kupigwa marufuku ametaja kuwa serikali sasa itaweka
sheria kali ya kutoa adhabu kali kwa watakaobainika wanajihusisha na biashara
haramu ya meno ya tembo ndani na nje ya nchi.
Waziri wa maliasili na utalii Lazaro
Nyalandu amesema wizara imeomba serikali kuajiri haraka askari wa wanyama pori wapatao 430 hadi mwezi
wa saba mwaka huu kufanya kazi katika mbuga zote za wanyamapori nchini..
Amefafanua kuwa pia serikali imeagiza
helkopita 3 aina nchini marekani kwa ajili ya kupambana na majagili wanaoua
tembo na kusafiri pembe za ndovu kwenda mataifa mengine.
0 comments:
Post a Comment