Mkuu wa mkoa wa
kaskazini pemba Dadi Faki Dadi amewataka wafanyakazi wa sekta ya umma kuheshimu
maamuzi ya serikali na kutojiingiza katika migogoro ya kijamii.
Amesema
wafanyakazi wa serikali wanapaswa kuwa kioo kusaidia mipango ya serikali na
kitendo cha wao kujiingiza katika migogoro ni kwenda kinyume na sheria za
uajiri.
Akizungumza na
wafanyakazi wa wizara mbalimbali wanaoishi katika shehia ya kambini na mchangamdogo
katika kikao cha kusuluhisha mgogoro unaoendelea amesema mgogoro wa kugombania
skuli katika shehia hizo unadaiwa
kuchangiwa na baadhi ya wafanyakazi wa serikali.
Dadi amesema
serikali haiwezi kuwafumbia macho wafanyakazi hao na hatua za kisheria na
kinidhamu zitachukuliwa.
Katika hatua nyengine
Dadi amemsimamisha kazi sheha wa shehia ya mchangamdogo kutokana na kuhusika
kushawishi wananchi kuendeleza mgogoro huo uliosababisha skuli hiyo kufungwa na
wanafunzi kukosa masomo.
0 comments:
Post a Comment