April 20, 2016

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma amesema upatikanaji wa vifaa vya teknolojia ya kisasa zaidi ni hatua muhimu kufika lengo la kufikia falsafa ya taifa ya elimu kwanza.
Akipokea msaada wa Computer 21 kwa ajili ya Vyuo vya Walimu na skuli mbili zinazofundisha mtaala wa teknolijia ya habari na mawasiliano Zanzibar amesema vifaa hivyo vitawsaidia walimu kupata maarifa, kutafuta misaada ya ufundishaji pamoja na kuangalia hatua zilizofikiwa katika nchi nyengine ili kuiga na kufikia malengo ya kukuza elimu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Zantel Benoit Janin na Mtendaji wa Millicom kanda ya Afrika Bi. Cynthia Gordon, wamesema msaada huo wametoa ili kuiunga mkono SMZ katika kuimarisha teknolojia ya habari na mawasiliano kuanzia ngazi ya chini ili kufikia lengo la kuwa na idadi kubwa ya wataalamu watakaochangia maendeleo ya Zanzibar.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma



0 comments:

Post a Comment