Baraza la Tiba asili na tiba mbadala limeyafungia
maduka sita yanayouza dawa za miti shamba baada ya kubainika kuwa hayajafanya
usajili kwa kipindi kikubwa pamoja na kukiuka taratibu za baraza hilo.
Hayo yamebainika kufuatia kufanyika ziara ya
kushtukiza katika maeneno mbali mbali ya Mjini Magharibi na kugundua kuwa
baadhi ya wamiliki wa maduka ya dawa za miti shamba hawafuati taratibu zinazotakiwa katika uuzaji
wa dawa zao.
Mrajis wa Baraza hilo Haji Juma Kundi amesema katika
ukaguzi walioufanya jumla ya maduka ya dawa za tiba asili 16 na clinic tatu
walizikagua na kugundua kasoro mbali mbali ikiwemo uchafu pamoja na kutokuwa na
mpangilio mzuri wa dawa hizo.
Amesema kuna baadhi ya maduka ya tiba asili wamiliki
wao hawajafunga mikataba kwa kipindi cha
miaka mitano ya kuendesha biashara zao jambo ambalo ni kinyume na taratibu za
baraza hilo.
Kwa upande wa Cliniki zilizokaguliwa kumeonekana na
changamoto kadhaa zinazohatarisha afya za wanaokwenda kupata huduma hizo
ikiwemo kliniki Madawa Herbalist iliyopo maeneo ya Kijichi ambayo majengo yake
yanahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuweza kukidhi haja za wananchi.
Amesema changamoto nyengine ni kutokuwa na mpango
mzuri wa kuweka dawa zao, uchafu pamoja na kutokuwa wataalamu wa kuendesha
baadhi ya kliniki hizo.
Amewataka wamiliki wa cliniki za tiba asili na tiba
mbadala pamoja na wenye maduka ya tiba asili waganga pamoja na wenye vilinge kujisajili
katika baraza lao sambamba na kuchunguzwa dawa zao kwa Bodi ya chakula Dawa na
Vipodozi ili waweze kuwahudumia wananchi kwa uhakika na kuepusha matatizo ya
kiafya.
0 comments:
Post a Comment