Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka
wafanya biashara wa Tanzania kushirikiana na wafanya biashara wa Omani katika
kuwekaza katika viwanda ili kuleta ajira na kupunguza umaskini nchini.
Akifungua
mkuatano wa siku moja kibiashara kati ya wafanyabiashara wa Tanzania na Oman jijini Dar es salaam amesema uwezekekano wa
kufanya biashara na nchi ya Omani ni vyema fursa hiyo kutumiwa.
Waziri
wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage amesema Serikali imejipanga
kutengeneza ajira za kutosha kutokana na uwekezaji wa kibiashara uliopo kati ya
nchi hizo mbili.
Nae
Waziri wa Viawanda na Biashara wa Omani Dkt Ali Masoud Ali Alsunaidy amesema engo kubwa la mkutano huo ni kuwasukuma
wafanya biashara wadogo pamoja wajasilimia mali ili kufikia malengo yao.
Mkutano
huo wafanya biashara hao watapa fursa ya kujadili maeneo wataweza kushirikiana
kati yao na ni takriba wafanya biashara 300 wa Tanzania na Omani wameshiriki
katika mkutano huo.
0 comments:
Post a Comment