Zoezi la Upigaji dawa
Majumbani kwa ajili ya kuuwa mbu waenezao Malaria limenza rasmi
kisiwani Pemba ambapo Jumla ya Nyumba
31,369 zitapulizwa Dawa katika Wilaya ya Micheweni na Wilaya Ya Chake
chake.
Taarifa zilizotolewa na Mratibu wa Kitengo cha Upigaji dawa Kisiwani Pemba Khamis Salim
amesema zoezi hilo litafanyika katika Shehia 4 za Wilaya ya
Michweni na Shehia Moja Wilaya ya Chake kuanzia tarehe 1/3/2016 hadi tarehe 14/3/2016 na linaendeshwa na Shirika la ABT la Marekani kwa kushirikiana
na Kitengo cha kupambana na Malaria Zanzibar (ZAMAP) linanza Rasmi .
Amezitaja shehia
zinazohusika ni Makangale ,Mgelema, Tumbe Mashariki, Chimba na Shumba vyamboni.
Mratibu Salim amesema kuwa kigezo
kikubwa kilichotumika kuzipuliza dawa shehia hizo ni kesi
nyingi zilizopatikana katika Maeneo hayo yaliyokuwa sugu katika
kupambana na Malaria , licha ya Juhudi kubwa zinazochukuliwa
kukabiliana na hali hiyo.
Amewaomba wananchi kushirikiana na wapiga dawa
majumbani kwa kuruhusu nyumba zao kupigwa dawa vyumba vyote na waache tabia ya ujanja
wakutaka wapigiwe dawa baadhi ya vyumba pekee.
Mratibu Salim amefahamisha
kuwa zoezi hilo haliwezi
kufanikiwa iwapo Wananchi tasisi za Serikali na asasi za
kiraia hawatotoa ushirikaiano wao wa dhati katika
kuitokomeza malaria ambayo imekua ikisababisha vifo
vingi hasa watoto chini ya umri wa
miaka mitano
0 comments:
Post a Comment