March 01, 2016

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein amesema juhudi kubwa zilizochukuliwa na serikali katika kuimarisha  miundombinu ya sekta ya afya zimefanikisha utoaji wa huduma za matibabu  kwa wananchi mijini na vijijini.
Amesema hatua hiyo inatoa fursa nzuri kwa wananchi kupata huduma  za uhakika  za afya bila ya usumbufu ikilinganishwa na zilivyokuwa zikitolewa miaka michache iliyopita.
Dr. Shein amesema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi wa  mkutano wa tathmini ya mapitio ya pamoja  ya sekta ya afya  iliyosomwa na makamu wa pili wa rais  wa Zanzibar  Balozi Seif Ali Iddi nje kidogo ya mjini Zanzibar.
Amefahamisha kuwa hatua hizo ina lengo la kuona huduma za afya zinapatikana kwa wananchi si zaidi ya kilomita tano karibu na maeneo wanayoishi hasa vijijini.
Hata hivyo Dr. Shein ameeleza kuwa ujenzi wa majengo mapya  ya afya na uwepo wa vifaa bora vya matibabu hautatimia iwapo mipango ya muda mfupi na mrefu haitawekwa katika kuwapatia taaluma ya kisasa watendaji wa sekta hiyo muhimu.
Akigusia upatikanaji wa dawa mbali mbali Dr. Shein amesema katika serikali ya Zanzibar  imeongeza bajeti kutoka Shilingi bilioni 1.0 hadi Shilingi bilioni 4.3 mwaka 2015/2016 ili kukabiliana na upungufu wa huduma hiyo.
 Dr. Shein ameishauri Wizara ya Afya kuendelea kusimamia vyema mipango  iliyoiweka ikiwemo ile inayofadhiliwa na  washirika wa maendeleo ambayo itawawezesha watendaji wa sekta hiyo kutoka huduma kitaalamu zaidi.
Amewataka washiriki wa mkutano huo  wa mapitio ya pamoja  ya sekta ya afya wakiwemo madaktari waliobobea, wataalamu wa masuala ya mazingira wa ndani na nje ya nchi kutumia nafasi yao kitaalamu katika kutathmini sekta hiyo na kutoa ushauri  na muongozo yao katika kufikia viwango vinavyokubalika kitaifa na kimataifa..
Mapema Mwakilishi wa Taasisi na Mashirika Hisani ya Kimataifa yanayotoa huduma Nchini Tanzania Dr. Christin Harmel aMEsema  ni muhimu hudujma za afya ya msingi lazima ziendelee kuimarishwa ili kuwa na jamii yanye afya na uwezo wa kufanya  kazi za uzalishaji mali utakaosaidia mapato ya taifa.
Amesisitiza watendaji wa afya kuhakikisha  kila motto anayezaliwa mikononi mwao ni lazima alindwe, ahifadhiwe na kutunzwa katika mazingira bora yatakayomuwezesha kukua kwa amani na upendo.
Akimkaribisha mgeni rasmi kuufungua Mkutano huo Naibu Waziri wa Afya
Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo aMEyashukuru Mashirika na Taasisi za Kimataifa na zile za  Kitaifa Kwa mchango wo mkubwa ulioiwezesha Wizara ya Afya kufanya kazi zake kwa ufanisi mkubwa.

Mkutano huo unaozungumzia tathmini ya mapitio ya pamoja  ya Sekta ya Afya Zanzibar  umeoshirikisha Wataalamu na Washirika wa Maendeleo kutoka Taasisi za Kimataifa na Kitaifa umefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya.

Mwakilishi wa Taasisi na Mashirika Hisani ya Kimataifa yanayotoa
 huduma za afya Nchini Tanzania Dr. Christin Harmel akitoa salamu
 kwenye Mkutano wa Tathmini ya mapitio ya Sekta ya Afya.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dr. Saleh Mohammed Jidawi akitoa
maelezo ya ufafanuzi kwenye Mkutano wa Tathmini ya mapitio
ya Sekta ya Afya hapo Zanzibar Beach Resort Mbweni.

 

Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi
wa mashirika na taasisi za Kimataifa na zile za
kitaifa zinazotoa huduma ya Afya Zanzibar.

0 comments:

Post a Comment