March 18, 2016

Umoja wa Vyama visivyo na wakilishi Bungeni umewaomba wananchi wa Zanzibar kushiriki uchaguzi wa marejeo wa Jumapili ijayo kwa hali ya amani na utulivu ili kila moja aweze kutumia haki yake ya msingi.
Umesema kuwa hiyo ndio fursa pekee ya kuwapata viongozi wapya watakao uongoza nchi kwa kipindi cha miaka mitano.
 Wakizungumza na waandishi wa habari juu ya ushiriki wao katika uchaguzi mwenyekiti wa umoja huo Ali Kaniki amesema kurejewa uchaguzi kusiwe chanzo cha machafuko ya kisiasa  nchini hasa  kwa wale  wasiotakia mema  taifa.
Amesema vyama hivyo vimeamua kushiriki uchaguzi huo wa marejeo na  hawana pingamizi na maamuzi yaliyotolewa na tume ya uchaguzi Zanzibar kwa kuwa ule wa awali ulifutwa kisheria.
Amesema chama chochote cha siasa kazi yake ni kushiriki uchaguzi na sio kususia kwani kufanya hivyo kutakosesha wananchi  haki yao ya msingi na  kurudisha nyuma shughuli za maendeleo.
Nae katibu mkuu wa umoja huo Rovatus Muabhi amefahamisha  wamechukuwa maauzi hayo  kwa mujibu wa sheria ya nchi na ni tofauti na inavyotangazwa kuwa wamerubuniwa na vyama vyengine vya kisiasa.
Makatibu hao wamesema kurejewa uchaguzi sio jambo geni duniani  na yapo mataifa mengi yamewahi kurejea uchaguzi kutokana na kasoro mbali mbali zilizojitokeza katika chaguzi zao.
Viongozi wa Umoja huo wamesema  pamoja na kushiriki uchaguzi pia wamesimamisha  wagombea  12 ambao wamo katika ngazi zote ikiwemo rais, wawakilishi na madiwani.

Vyama hivyo ni pamoja na vitakavyoshiriki katika marudiao ya uchaguzi huo ni DP, CCK, AFP, DEMOKRASIA MAKINI, SAU, TLP, UPDP, UMD, ADC, NRA, TADEA NA CHAUMMA.
Mmoja wa wagombea Urais kwa tiketi ya chama cha TLP Hafidh Hassan Suleiman 
akithibitika wa kugombea na kuwataka  wananchi kumpikia kura yeye. 
Picha Maelezo Zanzibar


0 comments:

Post a Comment